Tuesday 25 March 2014

TAARIFA KWA WALIMU WAPYA KABLA YA KURIPOTI KWENYE VITUO VYAO VIPYA VYA KAZI.

Ndugu wadau wa taaluma hii ya ualimu kwanza nipende kutoa pongezi kwa wale wote ambao wameweza kupangiwa vituo vyao vipya vya  kazi,haijalishi umepangiwa wapi na serikali ila kikubwa ni kupata nafasi ya kazi kwanza na mengine ndio yatafata baadae.

Pia napenda kutoa pole kwa wale wote ambao mpaka sasa hawajayaona majina yao ila bado wanayasubiri.Naomba mzidi kuwa na subira juu ya hilo ingawa inaumiza sana.

Leo nimeona ni vyema kuwapa taarifa muhimu wale wote ambao wamepata nafasi katika vituo vyao vipya vya kazi ya kufundisha.

Haya ni mambo muhimu yakuzingatia kabla hujaripoti kwenye kituo chako kipya cha kazi:

1.Mpaka sasa halmashauri nyingi zimeshatoa majina ya shule unayotakiwa kufundisha.Kwahiyo kwa wale wote ambao majina yao yalitolewa bila kuonesha umepangiwa shule gani,unaweza kuwasiliana na mtu yeyote aliye kwenye halimashauri husika akuchekie jina lako kwenye mbao za matangazo za hiyo halmashauri ili ujue umepangiwa shule gani.
Kama halimashauri yako hawajayaweka basi ni maswala yao tu ya utendaji huenda hayajakaa vizuri.



2.Kuna vitu vya kubeba ambavyo vinatakiwa kuwasilishwa kwenye shule husika,navyo ni kama vifuatavyo:

  • Cheti chako cha kuzaliwa.
  • Cheti chako cha kidato cha nne.
  • Cheti chako cha kidato cha sita kama utakuwa nacho maana kuna wengine waliunga diploma baada ya kumaliza certificate.
  • Cheti chako cha chuo pamoja na transcript. 

3.Pia unaweza kubeba picha za passport size za ndugu zako au watu wako wa karibu unaotaka watengenezewe vitambulisho vya bima ya afya.Maana huwa kwa kawaida ni watu 6 ukiwa na wewe.Kubeba passport zao mapema itakusaidia kuokoa gharama za kuzituma tena wakati zinapohitajika maana natumai utakuwa mbali nao.


Mwisho niwatakie kila lakheri katika utendaji wenu mpya wa kazi.

2 comments:

  1. Kwanza tunaishukuru blog hii kwa kutujuza mambo mbalimbali mapya yanayojiri kila cku.Pili tukushukuru wewe mwenye blog





























    mh.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nawashukuru sana kwa kuweza kunieleza hayo maana si wote wanaweza kukwambia uzuri wa kazi zako.Naahidi kuwa pamoja na wasomaji wangu kwa habari zote zenye kuweza kuisaidia na kuikomboa jamii

      Delete