Monday 14 April 2014

SERIKALI YASHINDWA KUANDAA MIPANGO YA KUDHIBITI MAJANGA KABLA YA MVUA

Siku kadhaa zilizopita,serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania ilitangaza hali ya hatari kwa wananchi wake hususani wale waishio maeneo ya mabondeni.Serikali ilisema itanyesha mvua kwa siku kadhaa kwahiyo wananchi wa maeneo hususani ya mabondeni wanatakiwa kuhama kabla ya mvua hiyo kubwa kunyesha na kuwaletea madhara makubwa.

Siku za mbeleni baada ya tamko hilo,mvua kubwa ilinyesha na kusababisha madhara makubwa sana kwa mali na hata vifo kwa baadhi ya watu na upotevu wa vitu na watu pia.Sio hayo tu bali hata barabara nyingi nazo zilishindwa kupitika kutokana na hali hiyo,mfano kutokea ubungo jijini Dar es Salaam kwenda mikoani,kipande cha mlandizi na mto ruvu koote palikuwa hapapitiki kabisa na njia zilifungwa kwa mda.

Magari yalizuiliwa kupita kabisa na vyombo vya dola hapo mlandizi na Ruvu ili kuepusha maafa zaidi.Viongozi mbalimbali waliweza kufika mfano, mkuu wa mkoa wa Pwani Bi Mwantumu Mahiza nae alikuwa miongoni mwa viongozi hao ambaye nilimshuhudia mimi mwenyewe.

Baadhi ya wasafiri waliokuwepo jana,eneo la Ruvu na Mlandizi, waliweza kumuhoji ili kujua nini njia mbadala ya kufanya ili kujinusuru kwa mda huo,maana magari yalizuiwa kwa mda,alijibu yafuatayo

"Kama humuwezi kurudi Ubungo basi mtakuwa wenyeji wa mkoa wa Pwani na mnakaribishwa kama wageni wa mkoa huu."
Wananchi waliona ni dharau sana kwa kiongozi kama huyo kutoa kauli hiyo bila kujali hasara waipatayo hapo.

Msikilize zaidi hapa alichonena jana,


Serikali imeweza kutangaza hali ya hatari kwa wananchi wake lakini imeshindwa kuaandaa njia mbadala ya kukabiliana na majanga hayo na pia imesahau kuwa sio watu wote wanasikiliza na kuangalia vyombo vya habari kutokana na shughuli zao mbalimbali za kujipatia kipato zinavyowatinga.

Ni vyema serikali ikitangaza hali ya hatari basi pia itangaze na kujiandaa jinsi gani ya kuweza kuwasaidia wananchi wake katika kuepukana na athari za majanga hayo.


Picha zaidi hizi hapa

NJIA YA RUVU NDIVYO ILIVYOZIBWA NA MAJI,JANA NA KUTORUHUSU KUPITA KWA MAGARI MENGI HUSUSANI YAENDAYO MIKOANI







HAWA NI BAADHI YA NYOKA WALIOKUWA NJIANI WAKATI WANANCHI WALIPOKUSANYIKA HAPO KATI YA RUVU NA MLANDIZI JANA




KWENYE PICHA ZA CHINI ALIYEVAA MIWANI NDIO MKUU WA MKOA WA PWANI











HAYA NI BAADHI YA MAGARI LALIYOZUILIWA KUPITA KUELEKEA MIKOANI KUTOKEA DAR



HILI NI GARI LA KIKOSI CHA POLISI KWAAJILI YA USALAMA WA RAIA WA HAPO