Wednesday 26 February 2014

UZINDUZI WA KAMPENI YA UELEWA WA RASIMU YA KATIBA WAKAMILIKA

Leo tarehe 26/2/2014,ndani ya ukumbi wa Mlimani City,uliopo jijini Dar Es Salaam,kumeweza kufanyika rasmi Uzinduzi Wa Kampeni ya Uelewa wa Rasimu ya Katiba.

Uzinduzi huo umeweza kuwashirikisha wadau mbalimbali kama LHRC,wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho cha sheria na Haki za Binadamu, Dr Helen Kijo-Bisimba, Policy Forum,SHIVYAWATA,TYC na National Council Of NGOs (NaCoNGO), TUCTA,Jukwaa La Katiba,TAWLA,TAMWA n.k.

Uzinduzi huo uliweza kuzindua mambo yafuatayo:

  • Kipeperushi cha mambo 7 makubwa mapya ya kuungwa mkono na wananchi katika rasimu ya katiba na mambo makubwa 5 yanayokosekana katika rasimu ya katiba.
  • Chapisho la lugha nyepesi
  • Tovuti tofauti tofauti
  • CDs na flash kwaajili ya kusikiliza rasimu ya katiba
  • Chapisho la nukta nundu kwa walemavu (Maandishi yanayosomwa na watu wasioona),na mambo mengine mengi
Katika swala la tovuti,wameweza kuzindua tovuti ifuatayo ambayo kwa sasa kila mtu popote alipo duniani ataweza kusoma vizuri mambo yanayoendelea kwenye mchakato wa kuipata katiba mpya.

Tovuti hiyo ni, http://www.taifaniletu.blogspot.com/

Pia wameeleza kwa baadae kidogo watakuwa na tovuti iitwayo www.sikilizarasimu.com ambayo nayo itasaidie kuelewa mabo yote ya rasimu ya katiba mya.


Wameeleza pia wataweza kuzunguka nchi nzima katika kutoa elimu ya maswala ya katiba kila mkoa ndani ya kata 3 za kila wilaya zenye watu wengi na kisha kuwasambazia watu wengine.



No comments:

Post a Comment