Wednesday 19 February 2014

Tembo Wadogo Nao Hatarini Kutoweka.


Jeshi la polisi mkoani Singida,limefanikiwa kumkamata kijana mwenye umri wa miaka 26 ambaye ni mkazi wa Ukombozi iliyopo Singida,akiwa na vipande16 vya meno ya tembo vyenye thamani ya zaidi ya milioni 17.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake,kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Singida SSP Cordula Lyimo,amesema kijana huyo alikamatwa baada ya jeshi la polisi kufanya msako kwenye kizuizi kilichopo kijiji cha Ukimbu wilaya ya Manyoni mkoani Singida.

Kijana huyo ambaye alikuwa ndani ya bus aina ya scania alikutwa na vipande hivyo ndani ya begi lake la nguo katika harakati za kutaka kuwatoroka askari ambapo juhudi zake zilishindwa kufanikiwa baada ya askari hao kumtilia mashaka na kuwahi kumkamata.

Pia amesema kwa sasa majangili wameamua kutumia mbinu mpya ya kuuwa tembo wadogo baada ya wale wakubwa kupungua kwa kasi kama alivyofanya kijana huyo aliyekamatwa.

Kwa sasa jeshi la polisi linaendelea na msako wa mtandao unaohusika na ujangili huo.






Source: ITV

No comments:

Post a Comment