Tuesday 11 February 2014

Kwanini walemavu hawa wamesahaulika???

Mpaka sasa Mh. Rais,Jakaya Kikwete,ameweza kuteua wajumbe wengine 201 kutoka asasi mbalimbali kama za Wafugaji,Wakulima,Walemavu wa ngozi,Wanasiasa,Taasisi za kidini,Wanaharakati mbalimbali n.k, ambao watajumuika na wabunge wengine katika kujadili juu ya uundwaji wa katiba mpya.

Bunge hili la katiba ambalo linategemewa kuanza tarehe 18-02-2014 bungeni Dodoma,lina lengo la  wajumbe kutoa maoni ambayo yanawakilisha wa Tanzania wengi juu ya muundo wa katiba mpya ambayo inategemewa kuanza kutumika 2015.Na baada ya hapo rasimu hiyo ya pili itarudishwa kwa wananchi ili kupigiwa kura za ndio au hapana,yaani wanaikubali au wanapingana nayo???.
Na kama itakubalika basi ndio itakuwa katiba mpya ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Cha ajabu mpaka mchakato wa kuteua wajumbe wa bunge la katiba kukamilika,kundi la walemavu wa masikio (Viziwi),hawakujumuishwa kwenye bunge hilo la katiba mpaka leo hii,tarehe13-02.

Wakiongea jana na ITV,wadau mbalimbali wamelaani kitendo hicho cha Mh. Rais kuwaacha watu hawa.
Vilevile hawakuishia hapo tu,wameongeza kwa kusema hata kwenye kituo cha kurusha matangazo ya bunge TBC 1, huwa wanakoseshwa haki ya kuelewa nini kinachoendelea maana hawawekewi mkalimani wa kuwatafsiria.
Wadau mbalimbali wamehoji kitendo hicho cha kundi hili kusahaulika ni kuwakosesha haki yao ya msingi kama watanzania.

Pia kwa kituo cha kurushia matangazo cha taifa TBC 1,ambacho kinaendeshwa kwa gharama ya pesa za walipa kodi,wanaona serikali haiwatendei haki kwa autoworker mkalimani, maana hata wao kodi wanalipa sawa na watu wengine wa kawaida kwahiyo wana haki ya kujua nini kinachoendelea ndani ya nchi yetu Tanzania.

Nini maoni yako???

No comments:

Post a Comment