Friday 28 February 2014

TANZANIA KAMA NCHI,IMEJIPANGAJE KUKATAA MISAADA INAYOTOLEWA NA MATAIFA TAJIRI AMBAYO INAKUJA NA MASHARTI YENYE SERA ZA USHOGA??

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametia saini mswada wenye utata unaotoa adhabu kali kwa watakaopatikana wakishiriki mapenzi ya jinsia moja.


Rais Museveni alitia saini mswada huo nyumbani kwake katika hafla iliyoshuhudiwa na maafisa wakuu wa serikali pamoja na wandishi wa habari.
Mswada huo ambao sasa utakuwa sheria, unatoa adhabu ya kifungo cha maisha jela kwa wale watakaopatikana na hatia ya kuhusika na mapenzi ya jinsia moja.


Mswada huo pia umeharamisha wanaharakati kutangaza misimamo yao hadharani kuhusu au kuwasaidia wanapenzi wengine wa jinsia moja kujitangaza hadharani.

Adhabu hiyo pia itatolewa kwa wale wanaopatikana na hatia ya kuwahusisha watoto katika vitendo hivyo, walemavu au kumuambikiza mtu virusi vya Ukimwi katika mapenzi ya jinsia moja.

Mswada huo umepigiwa debe sana nchini Uganda, lakini mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu yameulaani.
Uganda imepuuzilia mbali shinikio za Marekani na nchi zengine za Magharibi kutopitisha sheria kali dhidi ya vitendo vya mapenzi ya jinsia moja.

Mswada huo umeweka sheria kali zaidi dhidi ya uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja kwa yeyote atakayepatikana akishiriki.

Usagaji pia umeharamishwa kwa mara ya kwanza na pia ni hatia kumsaidia mtu kushiriki mapenzi ya jinsia moja. Wanaharakati wa kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja wanasema wanajiandaa kwenda mahakamani kupinga sheria hiyo mpya.

Uganda ni miongoni mwa mataifa 30 Afrika ambayo yameharamisha mapenzi ya jinsia moja. Ni wiki jana tu ambapo Rais wa Gambia Yahyah Jammeh aliyesema mapenzi ya jinsia moja ni sumu kali mno.





Benki ya dunia imebana msaada wa dola milioni 90 kwa Uganda , siku chache tu baada ya Rais Yoweri Museveni kuishinisha sheriua mpya dhidi ya mapenzi ya jinsia moja.

Benki hiyo imesema kuwa inataka kufanya tathmini yake kuhakikisha kuwa malengo yake ya maendeleo nchini Uganda katika sekta ya afya, ambayo msaada huo ulikuwa unanuiwa, hayataathirika .

Sheria iliyoidhinishwa na Rais Yoweri Museveni, ilitiwa saini Jumatatu na inatoa adhabu kali kwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.

Wafadhili wengine tayari wameanza kusitisha misaada Uganda. Wahisani kama Denmark na Norway wamesema kuwa wataanza kufadhili mashirika moja kwa moja badala ya serikali.
Aslimia 20% ya bajeti ya Uganda inategemea michango ya wafadhili.


Mpaka sasa nchi tatu za Ulaya zimeamua kukata misaada yao kwa mamilioni ya dola.
Wizara ya fedha ya Uganda imesema inasubiri mawasiliano rasmi ya nchi husika, na iko tayari kukabiliana na athari za hatua hiyo.

Hadi kufikia sasa Waziri wa Fedha Wa Sweden, akiwa mjini Kampala, alisema wawekezaji kutoka nchi yake watakuwa na wakati mgumu kuweka pesa zao nchini Uganda kwa sababu watakuwa na hofu kuwa sheria yo yote inaweza kupitishwa kuwadhulumu watu.

Jana serikali ya Uholanzi ilisema itazuia kwa muda misaada kwa Serikali ya Uganda. Norway na Denmark pia zimetangaza kupunguza au kusimamisha kwa muda misaada yake kwa Uganda.





Marekani haikufurahishwa na hatua ya Uganda kuidhinisha sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja.


Waziri wa mashauri ya Kigeni wa Marekani, John Kerry amesema tangu Uganda iidhinishe mswada huo miaka minne iliyopita, Marekani ilieleza wazi kwamba sheria hiyo inakiuka jukumu la kuhakikisha kuwepo haki za binaadamu ambalo tume ya haki za binaadamu Uganda inatambua linaambatana na sheria ya Uganda.

Kerry amesema,' Baada ya kuidhinishwa sheria hii, tunaanza ukaguzi wa ndani wa uhusiano wetu na serikali ya Uganda, kuhakikisha kwamba pande zote za uhusiano wetu, ukiwemo miradi ya msaada, zinapinga sera na sheria zinazowaonea watu na tuwe na uhusiano unaodhihirisha maadili yetu'

Tamko hilo limetolewa siku moja baada ya rais Yoweri Museveni kukaidi shinikizo la kimataifa na kutia saini sheria hiyo iliyo zusha mzozo, inayoharamisha mapenzi ya jinsia moja Uganda, hatua iliyozusha hisia kali.

Baadhi ya mataifa ya magharibi tayari yanatishia kukatiza msaada wa moja kwa moja kwa serikali ya Uganda.



John Kerry
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Amerika John Kerry.




Marekani inasema kuidhinishwa kwa sheria hiyo kunatishia hatari ya kurudi nyuma katika uwajibikaji wa Uganda kulinda haki za raia wake na kutishia jamii ya wapenzi wa jinsia moja Uganda.


Waziri wa mambo ya nje nchini Uganda, Sam Kutesa amesema ana wasiwasi kuwa Marekani huenda ikasitisha msaada wake kwa taifa hilo baada ya Rais Yoweri Museveni kuidhinisha sheria dhidi ya ushoga nchini humo.
Bwana Kutesa amesema kuwa watu sharti wawe na maadili na kukubali msaada.
Balozi wa Marekani nchini Uganda Scott DeLisi, awali aliitaka serikali ya Uganda, kubatilisha sheria hiyo.
Alisema alihitaji kufafanuliwa zaidi sheria hiyo, kabla ya Marekani kujua ikiwa itaendelea na mipango yake ya misaada kwa nchi hiyo hasa miradi ya kupambana dhidi ya HIV na Ukimwi..

Sheria hiyo mpya, inatoa adhabu kali kwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja na kupiga marufuku kile inachosema kusambaza vitendo vya ushoga.






SOURCE: BBC SWAHILI



Hivyo ndivyo vikwazo walivyoanza kuvipata jirani zetu wa Uganda.

Tanzania kama nchi ambayo bajeti yake kubwa inategemea fedha za hao hao wafadhili kutoka nchi za magharibi amabazo ndio sera zao kubwa ni kuunga mkono ndoa za jinsia moja, imejipanga vipi kukabiliana na hilo????


Leo hii,viongozi wana mikakati gani kuimarisha uchumi ili swala la ushoga lisije likaharibu maadili ya nchi yetu???


Ni vyema kama taifa likaanza sasa maana wahenga wanasema,Ukiona Mwenzio Ananyolewa,Wewe Tia Maji.

No comments:

Post a Comment