Wednesday 11 June 2014

TUNAENDA KUTIBU MAGONJWA AU KUYAONGEZA???? (YALIYOMO KWENYE HOSPITALI ZA SERIKALI)

Nchini Tanzania hususani hospitali za serikali huduma za afya zimekuwa sio nzuri kabisa.Hospitali nyingi zinajulikana kama ni za serikali kwa majina lakini kiutendaji wake ni za kibinafsi (private hospitals).

Ukienda madawa mengi hakuna na utaelekezwa kwenda kuyanunua kwenye maduka ya madawa ambayo mengi yao ni ya hao madaktari wanaokuelekeza.Kinachofanyika wanayachukua madawa ya hospitali za serikali na kuyaweka kwenye maduka yao binafsi.

Pia kuna kamchezo huwa wanafanya wauguzi,yaani unaandikiwa dawa nje na zile alizokuandikia daktari kwenye kakaratasi kidogo na unazinunulia hapo hapo hospitali.Ukija kuwakabidhi unakuta hazitumiki zote kumbe zile ulizoandikiwa na hao wauguzi zinakuwa zao,nao wanaziuza kwa wengine.
Wakifanya hivyo kwa wagojwa kadhaa,mpaka watakapotoka wanajikuta wana hela nzuri tu za matumizi yao binafsi.

Wenye kutumia bima za afya nao hawapati huduma ipasavyo na hawapewi kipaombele kama wale wenye fedha taslim.Cash ndio inathaminiwa sana kuliko pesa ambazo kuzipata unatumia milolongo kadhaa.

Rushwa imetawala sana katika hospitali hizo,yaani wenye kuhonga sana hupata huduma nzuri na wale wa kidogo basi nao hupata kidogo ila wale wasionacho basi hukosa kabisa huduma nzuri.

Usafi katika hospitali hizi sio wa kuridhisha hususani vyooni.Kama inatokea mgonjwa anaumwa UTI na akapelekwa kwenye hospitali hizi,basi sanasana anaweza kuongeza tatizo pale anapotaka kwenda chooni kujisaidia.
Uchafu wa vyoo hivyo hukufanya kuahirisha haja yako au kutokwenda kabisa chooni na ikiwezekana unatafuta njia mbadala ya kutoa haja yako kama kwenye makopo au nje.

Pia kuna mrundikanoi mkubwa sana wa wagonjwa kwenye wodi zao na hii ni kwasababu ya vitanda vichache na wagonjwa kuwa wengi hivyo vitanda kutokidhi haja za wagonjwa.
Kwa kufanya hivyo wagonjwa wanakuwa rahisi kuambukizana magonjwa ya kuambukiza kama TB, n.k



AFYA NI SEKTA MUHIMU SANA YENYE KUHITAJI MABORESHO YA HALI YA JUU SANA.
BINADAMU BILA KUWA NA AFYA NZURI YOOTE HAYAWEZI KUFANYIKA IPASAVYO

No comments:

Post a Comment